MAHAKAMA YA ICC YAIDHINISHA UCHUNGUZI DHIDI YA MADAI YA UHALIFU YALIYOFANYWA KWA AMRI SERIKALI YA BURUNDI
TAREHE 10-11-2017
Majaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC
wameidhinisha uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu yaliyofanywa kwa amri ya
serikali nchini Burundi ambayo ni pamoja na mauaji, ubakaji na utesaji.
Majaji hao wamesema vithibitisho vilivyotolewa na
waendesha mashitaka vinatoa sababu ya msingi ya kuendelezwa kwa uchunguzi wa
makosa ya uhalifu yaliofanyika tangu Aprili 26 2015, yanayodaiwa kufanywa na
mawakala wa serikali na makundi yanayotekeleza sera ya serikali.
Burundi iliingia
katika ghasia na mamia ya raia kupoteza maisha mwaka 2015, baada ya rais Pierre
Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania awamu ya tatu ya urais,
ambayoalishinda. Matukio hayo ya uhalifu ayanadaiwa kutendwa na jeshi la polisi
la Burundi, usalama wa taifa, vikosi vya jeshi na makundi ya umoja wa vijana wa
chama tawala yajulikanayo kama Imbonerakure.
MAHAKAMA YA ICC YAIDHINISHA UCHUNGUZI DHIDI YA MADAI YA UHALIFU YALIYOFANYWA KWA AMRI SERIKALI YA BURUNDI
Reviewed by safina radio
on
November 10, 2017
Rating:
No comments