WANAJESHI NCHINI ZIMBABWE WAMUWEKA MUGABE KWENYE KIZUIZI CHA NYUMBANI.
TAREHE 16-11-2017
Wanajeshi wa
Zimbabwe wamemuweka rais Robert Mugabe kwenye kizuizi cha nyumbani katika hatua
inayoonekana kuwa wanajeshi hao wametwaa mamlaka ya nchi hiyo.
Hata hivyo meja
jenerali Sibusiso Moyo amesema lengo lao ni kuwakabili wahalifu wanaomzunguka
rais Mugabe na sio kuipindua serikali. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
alizungumza na rais Mugabe na kuthibitisha kwamba kiongozi huyo wa Zimbabwe
anazuiliwa nyumbani kwake.
Akizungumzia juu ya
hali ya nchini Zimbabwe katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres ametoa
mwito wa utulivu na subira.
Rais wa Umoja wa
Afrika Alpha Conde amelaani hatua ya wanajeshi wa Zimbabwe ya kutwaa mamlaka ya
nchi hiyo,ambapo amewataka wanajeshi hao warejee kambini ili kuiheshimu katiba.
WANAJESHI NCHINI ZIMBABWE WAMUWEKA MUGABE KWENYE KIZUIZI CHA NYUMBANI.
Reviewed by safina radio
on
November 16, 2017
Rating:

No comments