DRINK WATER AITAMANI ENGLAND

Danny Drinkwater aonyesha nia ya kuichezea EnglandHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Danny Drinkwater ''anataka kuichezea'' England licha ya kutopokea simu ya kumtaka kushiriki mechi za kirafiki dhidi ya Ujerumani na Brazil , amesema kiungo wa kati wa zamani wa Leicester City Jamie Vardy.
Drinkwater , ambaye aliihamia Chelsea kwa kitita cha pauni milioni 35 msimu wa joto , alimwambia meneja wa England Gareth Southgate hakuwa katika hali swari kushiriki mechi hizo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, ameshiriki mechi 22 za ligi ya Premia kwa dakika chache msimu huu.
''Amekuwa akijaribu kupata wakati zaidi uwanjani ,'' amesema mshambuliaji Vardy.
Dinkwater , aliyeshinda vikombe vitatu vya mwisho kwa England mwezi Mei 2016, alishiriki mechi yake ya kwanza mwishoni mwa Oktoba baada ya kupatwa na jeraha la paja na kifundo cha mguu tangu kujunga na mabingwa hao mwezi Agosti.
''Alijeruhiwa na anahitajika kujikakamua zaidi ili kupata umairi wake tena. Amekuwa akifanya hivyo kwa wiki za hivi majuzi na Chelsea na anastahili kukazana na mazoezi , Aliongezea Vardy
Southgate amesema alikuwa amezugumza na Drinkwater hapo awali kabla mapumziko ya kimataifa na kiungo huyo wa kati alisema ''Hayuko tayari kucheza katika kiwango hicho.''
Meneja wa zamani wa Middlesbrough aliongezea: iwapo Danny hakujihisi kama yuko tayari ningeelewa kwa kiwango cha wakati alichokuwa nacho na hakushiriki mechi mwishoni mwa msimu alipokuwa na Leicester pia.''
DRINK WATER AITAMANI ENGLAND DRINK WATER AITAMANI ENGLAND Reviewed by safina radio on November 13, 2017 Rating: 5

No comments