WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHANDISI ISACK KAMWELWE AMESEMA SERIKALI IMEFANIKIWA KUTOKOMEZA MAGONJWA YA MILIPUKO.
TAREHE 29-11-2017
Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Serikali imefanikiwa kutokomeza
magonjwa ya milipuko katika maeneo ya Kilimahewa, Kitangire na Kirumba katika
Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza baada ya zaidi ya kaya 300 kuunganishwa
katika mfumo wa maji taka.
Akizungumza
wakati wa kukagua utekelezaji wa mradi huo katika eneo la Kilimahewa, Waziri
Kamwelwe amesema kuunganishwa kwa Kaya hizo kwenye mfumo wa maji taka kumeondoa
tatizo la kutiririsha maji taka lililokuwa likichangia kuibuka kwa magonjwa ya
milipuko mara kwa mara.
Wakati huohuo
waziri huyo wakati akiwa jijini Mwanza amekabidhi magari matatu na pikipiki
sita kwa Wilaya za Misungwi, Magu na Busega kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji
wa miradi ya maji safi inayoendelea kwenye Wilaya hizo.
Miradi ya Maji
Safi pia inatekelezwa katika Miji ya Mwanza, Musoma na Bukoba ambapo
inatarajiwa kugharimu kiasi cha fedha shilingi bilioni mia mbili na arobaini na
tano ambazo zimetolewa na serikali ya Tanzania pamoja na wadau mbalimbali wa
maendeleo.
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MHANDISI ISACK KAMWELWE AMESEMA SERIKALI IMEFANIKIWA KUTOKOMEZA MAGONJWA YA MILIPUKO.
Reviewed by safina radio
on
November 29, 2017
Rating:

No comments