SHULE YA SEKONDARI YA KIMATAIFA YA MOSHI YA ISM MKOANI KILIMANJARO YATAKIWA KUWAPA MIKATABA WAFANYAKAZI WA SHULE HIYO.
2-11-2017
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,
bunge,vijana,ajira na watu wenye ulemavu Mh Antony Mavunde ameuagiza uongozi wa
shule ya sekondari ya kimataifa ya Moshi ISM iliyoko mkoani Kilimanjaro
kuwapatia mikataba isiyokuwa na muda maalumu wafanyakazi wote wa shule hiyo kwa
mujibu wa sheria.
Mh Mavunde ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea
shule hiyo na kubaini kuwa mikataba inayotolewa katika shukle hiyo kwa sasa iko
kinyume cha sheria hivyo inahitaji kufanyiwa marekebisho.
Amesema kuwa ofisi yake itafuatilia suala hilo kwa
karibu ili haki iweze kutendeka hasa kwa watanzania ambao wapo katika ajira ili
waweze kupata ajira za kudumu zitakazowapa uhakika wa kuendesha maisha yao.
Awali wakitoa malalamiko yao kwa naibu waziri huyo
wafanyakazi hao wamesema kuwa wanafanya kazi zao kwa hofu kutokana na kutokuwa
na uhakika wa ajira za kudumu katika eneo lao la kazi.
SHULE YA SEKONDARI YA KIMATAIFA YA MOSHI YA ISM MKOANI KILIMANJARO YATAKIWA KUWAPA MIKATABA WAFANYAKAZI WA SHULE HIYO.
Reviewed by safina radio
on
November 02, 2017
Rating:

No comments