WAKAZI WA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA UGONJWA WA KISUKARI NA KUJUA NAMNA BORA YA KUJIKINGA
TAREHE 14-11-2017
Ikiwa leo ni siku ya
maadhimisho ya siku ya kisukari duniani wakazi wa jiji la Arusha wametakiwa
kujitokeza katika vituo mbalimbali vya afya ili kupata vipimo vya ugonjwa huo
na namna ya kujikinga nao.
Ushauri huo umetolewa
na mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza mkoa wa Arusha Dr Rose Mende wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa
kisukari duniani ambayo inafanyika leo,ambapo amesema kuwa huduma ya kupata
huduma ya vipimo hivyo itatolewa katika wilaya zote za mkoa wa Arusha.
Dr Mende amesema kuwa huduma
hiyo ya upimaji itatolewa bure kwa watu wote watakaojitokeza kwa siku ya leo na ya kesho,ambapo mbali na kutolewa kwa vipimo
hivyo wataalamu wa afya pia watatoa elimu juu ya madhara na namna ya kukabilina
na ugonjwa huo ambao umekuwa ukiwapata watu wengi bila kujali umri wao.
Amesema kuwa katika
jiji la Arusha vituo vitakavyotumika kutoa huduma hiyo bure ni pamoja na
hospitali ya mkoa ya Mount Meru,kituo cha Afya Levolosi na viwanja vya azimio
la Arusha.
Hata hivyo maadhimisho
ya siku ya ugonjwa wa kisukari duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14
Novemba ya kila mwaka ambapo kwa hapa Tanzania watu wenye ugonjwa huo ni
asilimia 9.1 huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni Wanawake na kisukari haki
yetu kwa afya bora ijayo.
WAKAZI WA MKOA WA ARUSHA WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA UGONJWA WA KISUKARI NA KUJUA NAMNA BORA YA KUJIKINGA
Reviewed by safina radio
on
November 14, 2017
Rating:

No comments