WATU WAPATAO 28 WAMERIPOTIWA KUUAWA KATIKA MAANDAMANO NCHINI ERITREA
1-11-2017
Watu
wapatao 28 wameripotiwa kuuawa na wengine 100 wamejeruhiwa katika maandamano
yaliyofanyika kwenye mji mkuu wa Eritrea, Asmara.
Kundi
kubwa la upinzani nchini humo la Red Sea Afar Democratic Oganization,
limewaambia waandishi habari kuwa maandamano hayo yalikuwa makubwa na kwamba watu kadhaa wamekamatwa.
Ubalozi
wa Marekani nchini Eritrea umesema kuwa milio ya risasi ilisikika katika maeneo
kadhaa mjini Asmara kutokana na maandamano hayo.
Mwanasiasa mmoja wa upinzani amesema serikali
ya Eritrea ilijaribu kuidhibiti shule ya jumuia ya Waislamu, hatua
iliyosababisha ghasia hizo.
Kiongozi
wa muda mrefu wa Eritrea, Isaias Afewerki, ameitawala nchi hiyo tangu mwaka
1993, huku akiminya uhuru wa vyombo vya habari, kutofanyika kwa uchaguzi pamoja
na kudhibitiwa kwa uhuru wa kidini.
WATU WAPATAO 28 WAMERIPOTIWA KUUAWA KATIKA MAANDAMANO NCHINI ERITREA
Reviewed by safina radio
on
November 02, 2017
Rating:

No comments