MKUU WA MAJESHI TANZANIA JENERALI VENANCE MABEO AMESEMA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA JWTZ LITATOA MAFUNZO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA ASKARI WAKE.
22-11-2017
Mkuu wa majeshi Tanzania Jenerali Venance Mabeo amesema
Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limejidhatiti kuhakikisha linatoa mafunzo kwa askari wake kuhusu maswala ya
Sayansi na Teknolojia katika kukabiliana na changamoto za ulinzi na usalama.
Jenerali Mabeo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kutoa
mafunzo ya shahada ya kijeshi yatakayotolewa na Chuo cha Kijeshi cha TMA cha
Monduli cha Mkoani Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha Uhasibu Mkoani Arusha.
Mkuu huyo wa Majeshi amesema kwa sasa dunia imepiga hatua
katika Sayansi na Teknolojia hasa katika masuala ya ulinzi hivyo lazima jeshi
la Tanzania liwe tayari kwa taaluma hiyo.
Aidha, Jenerali Mabeo ameongeza kuwa sayansi na
teknolojia inahitaji elimu kubwa ambapo katika mapigano ya Medali yanatumia
teknolojia ya kisasa hivyo jeshi linapaswa kusonga mbele na kwenda na wakati,
ili jeshi lisiweze kubaki katika kupambana na vitisho vya sasa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa Dk. Florence Turuka amesema mafunzo hayo yanaumuhimu mkubwa
hasa katika kipindi hiki ambapo Dunia inakabiliwa na changamoto ya Ugaidi,
mapambano ya dawa za kulevya pamoja na mazingira.
MKUU WA MAJESHI TANZANIA JENERALI VENANCE MABEO AMESEMA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA JWTZ LITATOA MAFUNZO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA ASKARI WAKE.
Reviewed by safina radio
on
November 22, 2017
Rating:

No comments