EMMERSON MNANGAGWA AWAHUTUBIA WAFUASI WAKE NCHINI ZIMBABWE

TAREHE 23-11-2017


Mtu anayetarajia kuwa rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amerejea  jana nchini mwake na kuhutubia wafuasi wake waliojawa na furaha, akisema nchi hiyo inafungua ukurasa mpya wa siasa zake.

Aidha, Mnangagwa amesifu namna jeshi lilivyosimamia mchakato wa kumuondoa madarakani mtangulizi wake Robert Mugabe kwa amani na utulivu, na kusema kinachoshuhudiwa nchini Zimbabwe ni mwanzo wa demokrasia kamili.

Hali kadhalika ameinyoshea  mkono jumuiya ya kimataifa akisema Zimbabwe inahitaji msaada katika kukarabati uchumi wake ulioporomoka.

Emmerson Mnangagwa alikuwa mshirika wa muda mrefu wa Rais Robert Mugabe, na anatuhumiwa kuhusika na utekelezaji wa visa vingi vya uhalifu, yakiwemo mauaji ya maelfu ya watu wakati wa makabiliano baina ya Mugabe na wapinzani wake wa kisiasa mnamo miaka ya 1980.


Hata hivyo Mnangagwa anatarajiwa kukamilisha muhula wa Rais Mugabe hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika mwaka ujao,ambapo Wabunge wa upinzani ambao wanasema chaguzi zilizopita zilikuwa na wizi wa kura, wametaka uchaguzi ujao uwe huru na wa uwazi
EMMERSON MNANGAGWA AWAHUTUBIA WAFUASI WAKE NCHINI ZIMBABWE EMMERSON  MNANGAGWA AWAHUTUBIA WAFUASI WAKE NCHINI ZIMBABWE Reviewed by safina radio on November 23, 2017 Rating: 5

No comments