ASKARI 10 NCHINI SUDANI WAUAWA

Askari 10 akiwemo kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la Sudan wameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka hivi karibuni katika jimbo la Darfur.

Waziri wa Ulinzi wa Sudan, Ali Mohamed Salem amenukuliwa na shirika rasmi la habari la serikali SUNA akisema kuwa, wanajeshi hao waliuawa baada ya gari lao kutekwa na kundi moja la waasi, katika wimbi jipya la mapigano lilioanza Jumapili iliyopita.

Haya yanajiri saa chache baada ya kikosi kimoja cha jeshi la Sudan kumtia nguvuni Musa Helal, kamanda wa kundi la waasi wa Darfur katika mkoa wa Darfur Kaskazini kwa tuhuma za kuvunja haki za binadamu.

Tangu mwaka 2003, jimbo la Darfur limekumbwa na machafuko na mapigano ya silaha huku makabila ya eneo hilo yakilalamika kuwa serikali imewabagua ambapo hadi sasa machafuko hayo yamesha sababisha vifo vya watu laki tatu na wengine takriban milioni mbili na nusu kuwa wakimbizi ndani na nje ya Sudan.


Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa zinaendesha operesheni ya kulinda amani katika jimbo hilo chini ya mwavuli wa kikosi cha UNAMID.
ASKARI 10 NCHINI SUDANI WAUAWA ASKARI 10 NCHINI SUDANI WAUAWA Reviewed by safina radio on November 28, 2017 Rating: 5

No comments