CHAMA CHA ANC KUFANYA UCHAGUZI KUMTAFUTA MRITHI WA RAIS JACOB ZUMA.
TAREHE 18-12-2017
Chama tawala cha Afrika Kusini, African
National Congress, ANC kinapiga kura ya kumchagua mrithi wa Rais Jacob Zuma.
Wachambuzi wanasema kinyang'anyiro cha uongozi
wa chama cha ANC ni kikali mno kati ya Makamu wa Rais Cyril Ramaphosa na mke wa
zamani wa Zuma na ambaye ni waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma.
Bontle
Mpakanyane kutoka tume ya uchaguzi ametangaza kuwa viongozi hao wawili ndio
wagombea pekee katika kinyang'anyiro cha mwisho.
ANC ilichelewesha uchaguzi huo kutokana na
mgogoro kuhusiana na wajumbe wanaoruhusiwa kushiriki katika zoezi hilo.
Hata hivyo Uchaguzi huo unafanyika wakati kukiwa na
kashfa na tuhuma za rushwa ambazo zimechafua mihula miwili ya urais wa Zuma na
chama cha ANC baada ya kuwa madarakani kwa miaka 23.
CHAMA CHA ANC KUFANYA UCHAGUZI KUMTAFUTA MRITHI WA RAIS JACOB ZUMA.
Reviewed by safina radio
on
December 18, 2017
Rating:

No comments