MKUTANO MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAPINGANA NA RAIS TRUMP

TAREHE 22-12-2017
n
Image caption
Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake.
Mataifa mia moja ishirini wameyapigia kura maazimio,  yakiwamo mataifa ambayo ni washirika wa karibu wa marekani kama  Japan, Uingereza na Ujerumani.
Canada na Mexico ni moja ya mataifa thelathini na tano ambayo hayakuhudhuria mkutano huo,ambao Wapalestina wamesema  hatua hiyo  ya Umoja wa mataifa kuwa ni ushindi wa Palestina ingawa Israel imeyakataa matokeo hayo .

Kabla ya kura hiyo  balozi wa marekani katika umoja wa mataifa, Bi Nikki Haley alionya kuwa Marekani haitasahau au kusamehe pale nchi zilizoipinga Marekani zitakapoenda kuomba misaada.
MKUTANO MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAPINGANA NA RAIS TRUMP MKUTANO MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAPINGANA NA RAIS TRUMP Reviewed by safina radio on December 22, 2017 Rating: 5

No comments