WAZIRI WA NISHATI MERNAD KALEMANI AMESEMA KUWA VIJIJI VYOTE KATIKA JIMBO LA MTERA KUPATA UMEME.
TAREHE 22-12-2017
Waziri wa nishati hapa nchini Mh Mernad Kalemani
amesema kuwa mradi wa uwekaji umeme vijijini awamu ya tatu itaweka umeme katika
vijiji na kata zote za jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Mh Kalemani ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya
kujionea kazi ya usambazaji umeme vijijini REA awamu ya tatu inavyoendelea
katika jimbo hilo pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Amesema mbali na mradi huo kuweka umeme kwenye
taasisi,mashirika,pamoja na masoko utawekwa pia kwenye nyumba za wakazi wote
ambao wameshalipia gharama za kuunganishiwa huduma hiyo bila kusahau makanisa
na misikiti.
Kwa upande wake mbunge wa Mtera Mh Livingstone
Lusinde amesema kuw akutokuwepo kwa umeme katika jimbo hilo imerudisha nyuma
jitihada za kuanzisha miradi mbalimbali za maendeleo.
WAZIRI WA NISHATI MERNAD KALEMANI AMESEMA KUWA VIJIJI VYOTE KATIKA JIMBO LA MTERA KUPATA UMEME.
Reviewed by safina radio
on
December 22, 2017
Rating:

No comments