NAIBU WAZIRI WA KILIMO NCHINI DK. MARY MWANJELWA ATOA SIKU SABA KWA MKURUGENZI WA BODI YA PARETO KUTOA MAJIBU YA KERO ZA WAKULIMA.

TAREHE 01 -12-2017


Naibu waziri wa Kilimo Nchini Dk. Mary Mwanjelwa ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto Nchini  kuhakikisha wanatoa majibu ya kero za wakulima wa zao hilo Wiliyani Mbeya ambao wamekosa imani na Bodi hiyo.

Dk. Mwanjelwa ametoa muda huo kufuatia malalamiko ya wakulima wa zao la pareto kukosa mtetezi licha ya serikali kuanzisha bodi hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima.

Aidha, Dk. Mwanjelwa amemwagiza Mkurugenzi wa Bodi hiyo ya Pareto nchini kutoa majibu ndani ya siku saba baada ya kufika Wilayani hapo.

Pia, Naibu Waziri huyo wa Kilimo ameongeza kuwa inapaswa suala hilo lifike mwisho na kuhakikisha jinsi ya kupanua wigo wa fursa za masoko kwa ajili ya kumbadilisha mkulima wa zao hilo la pareto.


Hata hivyo, Tanzania ni nchi ya pili Duniani na ya kwanza Barani Afrika kwa uzalishaji wa zao la pareto na asilimia 80 ya zao hilo huzalishwa Wilayani Mbeya.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO NCHINI DK. MARY MWANJELWA ATOA SIKU SABA KWA MKURUGENZI WA BODI YA PARETO KUTOA MAJIBU YA KERO ZA WAKULIMA. NAIBU  WAZIRI WA KILIMO NCHINI DK. MARY MWANJELWA ATOA SIKU SABA KWA MKURUGENZI WA BODI YA PARETO  KUTOA MAJIBU YA KERO ZA WAKULIMA. Reviewed by safina radio on December 01, 2017 Rating: 5

No comments