WAZIRI WA UJENZI MAKAME MBARAWA AMEWATAKA WAKANDARASI WANAOJENGA RELI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU.
TAREHE 13-12-2017
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa amewataka wakandarasi
wanaojenga reli ya kisasa yaani standard gauge kufanya kazi kwa uadilifu ili
kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati.
Waziri Mbarawa
ameyasema hayo mkoani Pwani wakati alipotembelea mradi huo katika kijiji cha
Soga ambapo pia ameitaka kampuni hodhi ya rasilimali za reli RAHCO kufuatilia
kwa karibu mradi huo ili ukamilike
ifikapo mwaka elfu mbili na ishirini.
Mh. Mbarawa amewataka
wakandarasi hao kufanya kazi kwa uadilifu na viwango walivyokubaliana na
serikali huku akiwataka wahandisi kuelewa kuwa wana wajibu mkubwa na chochote
kikiharibika katika mradi huo wa ujenzi wa reli wa kwanza kulaumiwa ni wao.
Mradi wa reli ya kisasa
unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa reli
kutoka Dar es salaam hadi Morogoro, na
ya pili kutoka Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma na utakuwa na urefu wa
kilomita mia saba ishirini na mbili na utagharimu kiasi cha shilingi trilioni
7.1.
WAZIRI WA UJENZI MAKAME MBARAWA AMEWATAKA WAKANDARASI WANAOJENGA RELI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU.
Reviewed by safina radio
on
December 13, 2017
Rating:
No comments