VYAMA VINAVYOUNGA MKONO KUJITENGA KWA JIMBO LA CATALONIA VYASHINDA UCHAGUZI.
TAREHE 22-12-2017
Vyama vinavyounga mkono jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania vimeshinda uchaguzi wa jimbo la Catalonia.
Vyama vinavyounga mkono jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania vimeshinda uchaguzi wa jimbo la Catalonia.
Ikiwa kura zote zinakaribia kukamillika
kuhesabiwa Katika uchaguzi ambao wapiga
kura wengi wamejitokeza vyama hivyo vinaonekana kushinda japo vimepunguza
kidogo idadi ya viti bungeni.
Matokeo hayo kwa vyovyote ni habari
mbaya kwa waziri mkuu wa Hispania,Mariano Rajoy ambaye aliingilia kati jimbo
hilo kujitenga hivi karibuni na kuitisha uchaguzi huo.
Akiwa uhamishoni mjini Brussels
aliyekuwa rais wa Catalonia ,Carles Puigdemont amepongeza matokeo hayo na
kusema ni ushindi wa demokrasia kwa sababu ya idadi kubwa ya watu walijitokeza
kupiga kura na kusema hakuna wa kuyapinga.
Hata hivyo baada ya uchaguzi huo tatizo
kubwa kwa pande zote ni kwamba hakuna uhakika kuwa uchaguzi huo na matokeo hayo
yanaweza kutatua mgogori huo unaoendelea baina ya Catalonia na serikali ya
Madrid.
VYAMA VINAVYOUNGA MKONO KUJITENGA KWA JIMBO LA CATALONIA VYASHINDA UCHAGUZI.
Reviewed by safina radio
on
December 22, 2017
Rating:
No comments