RAIS WA TANZANIA JOHN MAGUFULI AMEUTAKA UMOJA WA MATAIFA KUFANYA UCHUNGUZI KUBAINI CHANZO CHA VIFO VYA WANAJESHI 14.

TAREHE 14-12-2017


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa jeshi la ulinzi na usalama Mh John Magufuli ameutaka umoja wa mataifa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo kamili cha vifo vya wananjeshi 14 wa Tanzania waliouawa wiki iliyopita wakati wakilinda amani huko jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Mh Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika salamu zake zilizotolewa kwa niaba yake na waziri mkuu Mh Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa zoezi la kuaga miili ya wanajeshi hao liliofanyika katika viwanja vya jeshi jijini Dar-es-salaam.


Sherehe za kuwaaga wanajeshi wa TZ waliouawa DRC zafanyika
Image captionAmesema kuwa vifo vya walinda amani hao vimesababisha majonzi makubwa kwa watanzania hivyo ni lazima umoja wa mataifa ufanye uchunguzi wa kina na ulio wazi na haraka iwezekanavyo kuhusu vifo vya wananjeshi hao ili ukweli uweze kujulikana na haki iweze kutendeka.
Kwa upande wakae waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taaifa Mh Hussen Mwinyi amesema kuwa pamoja na vifo vya wananjeshi hao jeshi la Tanzania halitakata tamaa katika kutimiza wajibu wao kama taifa huko Kongo na maeneo mengine wanakotoa msaada wa kulinda amani.


Hata hivyo wanajeshi hao 14 wa Tanzania waliuawa wiki iliyopita baada ya kutokea shambulizi la kushtukiza lililofanywa na waasi huko nchini Kongo ambapo mbali na waliopoteza maisha wanajeshi wengine zaidi ya 40 walijeruhiwa katika tukio hilo.
RAIS WA TANZANIA JOHN MAGUFULI AMEUTAKA UMOJA WA MATAIFA KUFANYA UCHUNGUZI KUBAINI CHANZO CHA VIFO VYA WANAJESHI 14. RAIS WA TANZANIA JOHN MAGUFULI AMEUTAKA UMOJA WA MATAIFA KUFANYA UCHUNGUZI KUBAINI CHANZO CHA VIFO  VYA WANAJESHI 14. Reviewed by safina radio on December 14, 2017 Rating: 5

No comments