WAKURUGENZI WOTE HAPA NCHINI WAMETAKIWA KUTEKELEZA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA AFYA, MADARASA NA NYUMBA ZA WAALIMU.
TAREHE 18-12-2017
Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na
serikali na za mitaa Mh Suleman Jaffo amewataka wakurugenzi wote hapa nchini
kutekeleza miradi ya ujenzi wa vituo vya afya,madarasa,nyumba za waalimu na
mabweni ya wanafunzi kwa kutumia mfumo wa Force Account.
Mh Jaffo ametoa maagizo hayo baada ya kuridhishwa na
utekelezwaji wa zahanati,madarasa pamoja na maabara unaotekelezwa kwa kutumia
mfumo wa Force Account katika halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora
ambao kwa ujumla utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia sita hamsini na
moja.
Amesema kuwa wa mfumo wa Force Account ni mfumo unaowezesha
serikali kutekeleza miradi yake ya maendeleo kwa kutumia mafundi walioko katika
jamii badala ya wakandarasi wakubwa ambao hutumia gharama kubwa kujenga na
kutekeleza miradi hiyo.
Ameongeza kuwa kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na
wilaya ya Nzega kuanzia sasa wakurugenzi wa halmashauri zote hapa nchini
wanapaswa kutumia mfumo huo ili kuondoa matumizi mabaya ya fedha za serikali na
pia kuwapa ajira mafundi wa ujenzi walioko katika jamii ya kitanzania.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nzega Bw Godfrey
Mkopula ameahidi kusimamia ipasavyo fedha za miradi mbalimbali inayotengwa na serikali kwa maslahi ya wananchi wa wilaya
hiyo.
WAKURUGENZI WOTE HAPA NCHINI WAMETAKIWA KUTEKELEZA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA AFYA, MADARASA NA NYUMBA ZA WAALIMU.
Reviewed by safina radio
on
December 18, 2017
Rating:

No comments