RAIS WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI AMEITAKA BENKI KUU KUZIFUTA BENKI ZILIZOSHINDWA KUJIENDESHA HAPA NCHINI.

TAREHE 13-12-2017


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli ameitaka benki kuu ya Tanzania kuzifuta benki zote ambazo zimeshindwa kujiendesha katika sekta ya kifedha hapa nchini.

Mh Magufuli ameyasema hayo leo muda mfupi kabla ya kuzindua tawi jipya la benki ya CRDB lililopo katika jengo la LAPF mjini 
Dodoma,ambapo amesema kuwa benki nyingi zimekuwa hazifanyi vizuri katika sekta ya kifedha hivyo ni lazima benki kuu ianze kuzichukulia hatua ikiwemo kuzifungia kuliko kuzifumbia macho.

Aidha katika hatua nyingine rais Magufuli ameitaka benki kuu kudhibiti uingizwaji na matumizi holela wa fedha za kigeni hapa nchini kuanzia serikalini hadi kwa watu binafsi kwa kuwa matumizi ya fedha hizo zinaharibu uchumi wa ndani.

Pia Mh Magufuli amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na mabenki mbalimbali hapa nchini ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kiuchumi na kuwawezesha wananchi wengi zaidi kukopa katika benki hizo kwa riba nafuu ili waweze kujikwamua na umaskini.


Hata hivyo katika sherehe hizo rais pia alimkabidhi mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr Bilinith Mahenge kiasi cha shilingi milioni mia moja kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo.
RAIS WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI AMEITAKA BENKI KUU KUZIFUTA BENKI ZILIZOSHINDWA KUJIENDESHA HAPA NCHINI. RAIS WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI AMEITAKA BENKI KUU KUZIFUTA BENKI ZILIZOSHINDWA KUJIENDESHA HAPA NCHINI. Reviewed by safina radio on December 13, 2017 Rating: 5

No comments