WAZIRI WA NISHATI MH. MERNAD KALEMAN AMETOA SIKU 3 KWA MENEJA WA KUZALISHA UMEME KITUO CHA MTWARA KUREKEBISHA MIUNDO MBINU YA UMEME.

TAREHE 14-12-2017


Waziri wa nishati na madini Mh Mernad Kalemani ametoa muda wa siku tatu kwa meneja wa umeme kanda ya kusini pamoja na meneja wa kuzalisha umeme kituo cha Mtwara kurekebisha miundombinu ya umeme inayoenda maeneo ya wilaya za mkoa wa Lindi na mkoa wa Mtwara.

Mh Kalemani ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya umeme mkoani Mtwara ambapo amesma kuwa ni lazima wahusika kurekebisha miundombinu hiyo na kujiridhisha kama inafanya kazi ili wananchi wapate huduma hiyo ya umeme.

Amesema kuwa katika mkoa wa Mtwara kuna umeme wa kutosha lakini baadhi ya maeneo hayapati umeme na hiyo inatokana na baadhi ya miundombinu mibovu inayoendelea kukarabatiwa ili kuhakikisha umeme wa kutosha unakuwepo katika maeneo hayo.


Hata hivyo katika ziara hiyo waziri Kalemani ametembelea mitambo ya kuzalisha gesi asilia kutoka baharini kuja nchi kavu katika kituo cha mnazi bey kijiji cha Msimbati kwa ajili ya kuona kiwango cha gesi kilichopo kama kinatosheleza.

WAZIRI WA NISHATI MH. MERNAD KALEMAN AMETOA SIKU 3 KWA MENEJA WA KUZALISHA UMEME KITUO CHA MTWARA KUREKEBISHA MIUNDO MBINU YA UMEME. WAZIRI  WA NISHATI MH. MERNAD KALEMAN AMETOA SIKU 3 KWA MENEJA WA KUZALISHA UMEME KITUO CHA MTWARA KUREKEBISHA MIUNDO MBINU YA UMEME. Reviewed by safina radio on December 14, 2017 Rating: 5

No comments