IMEBAINIKA KUWA AJALI NYINGI ZA BARABARANI MKOANI MBEYA ZINASABABISHWA NA MADEREVA KUSHINDWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI.

TAREHE 06-12-2017


Imeelezwa kuwa ajali nyingi za barabarani zinazotokea mkoani Mbeya kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na madereva ambao hawafuati sheria za usalama wa barabarani.

Hayo yameelezwa na kamanda wa kikosi cha  usalama wa barabarani mkoa wa Mbeya Bw Leopad Fungu wakati akizungumza katika  mkutano uliowahusisha madereva wa bodaboda na pikipiki uliofanyika mkoani humo ambapo amesema kuwa ajali hizo zimekuwa zikipoteza maisha ya watu hasa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.

Amesema kuwa kwa mwaka 2016 jumla ya ajali mia nne na moja za Bajaji ziliripotiwa  ambazo zilisababisha vifo vya watu sabini,ambapo mkoa wa Mbeya ndio unaoongoza kwa ajali nyingi kati ya mikoa yote hapa nchini hivyo kuna haja ya kila mkazi wa mkoa huo kufuata sheria za usalama wa barabarani ili kupunguza ajali hizo.

Kwa upande wake afisa mfawidhi wa mamlaka ya nchi kavu na majini SUMATRA mkoa wa Mbeya Bw Denis Daudi amewataka waendesha Bodaboda na Bajaji kuzingatia alama za usalama wa barabarani sambamba na kudhibiti mwendo kasi ili kuhakikisha kuwa suala la ajali linakuwa historia katika mkoa wa Mbeya.

Kwa upande wa madereva waliohudhuria katika mkutano huo wamelishukuru jeshi la polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kwa elimu wanayoendelea kuitoa na nakuahidi kushirikiana na jeshi hilo ili kukomesha ajali za mara kwa mara mkoani humo.


IMEBAINIKA KUWA AJALI NYINGI ZA BARABARANI MKOANI MBEYA ZINASABABISHWA NA MADEREVA KUSHINDWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI. IMEBAINIKA KUWA AJALI NYINGI ZA BARABARANI MKOANI MBEYA ZINASABABISHWA NA MADEREVA KUSHINDWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI. Reviewed by safina radio on December 06, 2017 Rating: 5

No comments