TAREHE 11-12-2017 Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage cap
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amerushiwa maji na maziwa kufuatia kushindwa na Manchester City huko Old Trafford.
United walikasirika kutokana na kile walichokiona kuwa kusherehekea kupindukia kwa City kufuatia ushindi wa Jumapili wa bao 2-1 ushindi ambao umefungua mwanya wa pointi 11 kileleni.
Wachezaji wa City walisherehekea na mashabiki wao baada ya kipenga cha mwisho na maafisa wengine wakajaribu kumshawishi meneja Pep Guardiola kujiunga nao lakini akakataa.
Baada ya wachazaji kuondoka uwanjani inaeleweka kuwa Mourinho alilalamika akiwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo kabla ya kurudi kwa mahojiano.
Upande wa City ulijibu huku kipa wa Brazil Ederson akijibizana na Mourinho kwa lugha ya kireno.
MOURINHO ARUSHIWA MAJI BAADA YA KUCHAPWA MABAO 2-1 NA MANCHESTER CITY
Reviewed by safina radio
on
December 11, 2017
Rating: 5
No comments