WAFANYABIASHARA WA MADINI YA TANZANITE WATAKIWA KUTOKUNUNUA MADINI YASIYO NA CHETI.
Naibu waziri wa Madini Mh.Stanslaus Nyongo amewataka wafanya biashara wa Madini ya Tanzanite nchini kutonunua Madini yasiyokuwa na cheti cha uhalisia ili kukomesha uuzwaji wa Tanzanite bandia nchini.
Mh. Nyongo ametoa rai hiyo katika mnada wa Madini ya Tanzanite
uliofanyika siku tatu katika mji mdogo wa mererani ikiwa ni Mara ya
kwanza kwa mnada huo kufanyika katika mji huo tangu kuanzishwa shughuli za
uchimbaji wa Tanzanite, huku washiriki wakuu katika Mnada huo
wakiwa ni Kampuni ya Tanzanite one na Stamico ambapo kampuni mbili zilijitioa
kabla ya mnada kuanza kutokana na kushindwa masharti.
Aidha amesema serikali ilianzisha hatua ya utoaji vyeti vya
uhalisia(certificate of origin) kwa Madini ya Tanzanite lengo likiwa ni
kuzuia uuzwaji wa Madini bandia pamoja na utoroshwaji wa Madini hayo ambapo
amewataka wafanya biashara hao kutokununua Madini yasiyoambatana na cheti
cha uhalisia.
Amepongeza hatua ya rais kuagiza minada yote ya Madini
ya Tanzanite kufanyika katika eneo linalochimbwa Madini hayo ambapo kwa miaka
yote minada imekuwa ikifanyika nje ya eneo hilo jambo ambalo
halikuwanufaisha wazawa wa eneo hilo.
Kwa upande wake Kamishna wa Madini nchini Benjamini Mchuampaka
amesema kupitia mnada huo serikali imepata zaidi ya shilingi milioni mia moja huku Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro
ikitarajia kulipwa zaidi ya shilingi milioni mia tano kama kodi ya
huduma ambapo amesema jumla kuu kutokana na mnada huo ni kiasi cha
bilioni 3.
Naye mkuu wa mkoa wa manyara bwana Alexander Mnyeti amewataka
wamiliki wa migodi kuhakikisha wanalipa kodi stahiki kwa serikali ambapo
amesema serikali imekusudia kuwafutia leseni wale wote ambao hawalipi
kodi huku wakiwa wanaendelea na shughuli za uchimbaji.
WAFANYABIASHARA WA MADINI YA TANZANITE WATAKIWA KUTOKUNUNUA MADINI YASIYO NA CHETI.
Reviewed by safina radio
on
December 22, 2017
Rating:
No comments