POLISI 18 WAFARIKI KATIKA SHAMBULIO NCHINI SOMALIA.
Mtu mmoja amejitoa
muhanga katika chuo kimoja cha mafunzo ya kipolisi nchini Somalia na kuwaua
maafisa wa polisi 18.
Maafisa nchini humo
wanasema polisi hao waliokuwa katika mafunzo walikuwa wamekusanyika kwa ajili
ya gwaride la asubuhi katika mazingira ya chuo hicho kilichopo mjini Mogadishu
wakati shambulizi hilo lilipofanyika.
Watu wengine 15
wamejeruhiwa katika shambulizi hilo linaloshukiwa kufanywa na wanamgambo wa
kundi la Al Shabaab.
Hata hivyo Maafisa
wanasema idadi ya vifo ingeweza kuwa kubwa zaidi iwapo mshambuliaji huyo
angejitoa muhanga katikati ya mkusanyiko mkubwa wa watu.
POLISI 18 WAFARIKI KATIKA SHAMBULIO NCHINI SOMALIA.
Reviewed by safina radio
on
December 15, 2017
Rating:
No comments