TANZANIA YASHAURIWA KUUNGA MKONO MASOMO YA UJASIRIAMALI.
Tanzania imeshauriwa kuuunga mkono masomo ya ujasiriamali yanayotolewa
na taasisi mbalinbali kwani uwepo wa masomo au kozi hizo utachangia maendeleo
hasa kwenye sekta ya viwanda.
Hayo yamelezwa na profesa Emanuel Matiko ambae ni mkuu wa
chuo kikuu cha Arusha wakati akiongea kwenye maafali ya 11 ya chuo hicho.
Profesa Matiko amesema kuwa masomo pekee ya ujasirimali yanaweza
kuokoa nchi ya Tanzania kutoka uchumi wa sasa hadi kufikia uchumi wa juu hasa
kama yataungwa mkono na serikali
Amefafanua zaidi kuwa
baadhi ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo wamekuwa na dhana ya kutaka kujiajiri
wenyewe lakini wanashindwa na kuongeza ikiwa
serikali itawasaidia basi dhana ya uchumi wa viwanda ingefika sehemu ambayo
imekusudiwa.
Awali mgeni rasmi katika maafali hayo,ambae ni askofu mkuu
jimbo kuu la kaskazini mwa Tanzania kanisa la wadventista askofu
Godwin Lekundayo amesema kuwa vijana wanapaswa kujiajiri wenyewe na waondokane
na dhana kwamba wanapaswa kuajiriwa na serikali.
Askofu Lekundayao amesema kuwa kwa sasa ni ngumu serikali kuweza
kuajiri vijana wote wanaomaliza vyuo lakini endapo watatumia elimu ya
ujasiriamali watakayoipata kutoka vyuoni itawasidia kujiajiri kwani watatumia
elimu hiyo kuzalisha bidhaa na kuweza kufikia uchumi wa kati na hata kuanzisha
viwanda.
TANZANIA YASHAURIWA KUUNGA MKONO MASOMO YA UJASIRIAMALI.
Reviewed by safina radio
on
December 18, 2017
Rating:
No comments