RAMAPHOSA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA ANC.
TAREHE 19-12-2017

Makamu wa rais wa
Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha African
National Congress, ANC, baada ya kushinda kinyang'anyiro kikali ambacho
kimedhihirisha mipasuko mikubwa ndani ya chama hicho ambacho kiliongoza vita
dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Maelfu ya wafuasi wa Ramaphosa waliimba na
kupiga kelele kwenye jumba la mkutano wakati wafuasi wa mgombea aliyeshindwa,
Nkosazana Dlamini-Zuma wakionekana kukata tamaa.
Ushindi huo unamuweka
Ramaphosa katika nafasi ya kumrithi Rais Jacob Zuma, ambaye utawala wake
umekumbwa na kashfa za rushwa, kudorora uchumi na ongezeko la hasira ndani ya
chama hicho.
Wajumbe waliosafiri kutoka maeneo mbalimbali
ya Afrika Kusini walipiga kura yao baada ya kucheleweshwa mara kadhaa kwa
sababu ya kuibuka tofauti kuhusiana na nani alikuwa na haki ya kupiga kura.
Hata hivyo Rais Zuma
alijiuzulu kuwa kiongozi wa chama katika mkutano huo, lakini huenda akabakia
kuwa kiongozi wa taifa hadi uchaguzi wa mwaka wa 2019.
RAMAPHOSA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA ANC.
Reviewed by safina radio
on
December 19, 2017
Rating:
No comments