EVERTON YAZIDI KUNG'AA LIGI KUU ENGLAND.


TAREHE 19-12-2017
EvertonLahaanshaha sawirkaGETTY IMAGES
Image caption
Klabu ya Everton imeibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Swansea City katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Goodsonpark.
Wageni wa mchezo huo Swansea, ndio walianza kuzifumania nyavu za Everton kwa goli Leroy Johan Fer alifunga katika dakika ya 35.
Katika dakika ya 45, mshambuliaji kinda wa Everton Dominic Calvert-Lewin akasawazisha goli hilo baada ya mkwaju wa penati ya Wayne Rooney kuokolewa.
Kiungo Gylfi Sigurdsson akaongeza goli la pili katika dakika ya 64, Wayne Rooney akasawazisha makosa yake kwa kufunga goli la tatu kwa mkwaju wa penati na kufikisha jumla ya magoli 10, msimu huu.
Swansea baada ya kupoteza mchezo huo wanaendelea kuburuza mkia wakiwa na alama 12, wakiwa na wamecheza 18.
EVERTON YAZIDI KUNG'AA LIGI KUU ENGLAND. EVERTON YAZIDI KUNG'AA LIGI KUU ENGLAND. Reviewed by safina radio on December 19, 2017 Rating: 5

No comments