NAIBU WA WAZIRI WA ELIMU MH. WILLIUM OLE NASHA AMESEMA SERIKALI ITAENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU.
TAREHE 01-12-2017
Naibu Waziri wa Elimu Mh. Willium Ole
Nasha amesema kuwa serikali imeendelea kuwekeza katika elimu kwa kutoa kiasi
cha shilingi bilioni 427.54 kama mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya
Chuo Kikuu cha Mt. Agustino Tanzania Tawi la Arusha, Mh.Nasha amesema kati ya
fedha hizo zilizotolewa na serikali jumla ya shilingi bilioni 100.7 tayari
zimeshakwisha kutolewa kama mkopo kwa wanafunzi zaidi ya laki moja kwa mwaka wa
kwanza.
Aidha, amewataka maafisa mikopo kutimiza
wajibu wao kwa kutoa mikopo kwa wakati ili kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria
masomo yao vizuri na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa maafisa
ambao hawatatoa mikopo hiyo kwa wakati.
Pia, amewataka wanafunzi wanaotarajia
kujiunga na vyuo hapa nchini kuwa makini na kufuata miongozo inayotolewa ikiwa
ni pamoja na kuzingatia muda na wakati wa kufanya usahili.
Vile vile, amesema kuwa mmomonyoko wa
maadili umekuwa ni janga kubwa katika nchi kutokana na matumizi mabaya ya
mitandao ya kijamii hivyo amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata
kujiendeleza na kukuza uchumi wa taifa.
NAIBU WA WAZIRI WA ELIMU MH. WILLIUM OLE NASHA AMESEMA SERIKALI ITAENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU.
Reviewed by safina radio
on
December 01, 2017
Rating:

No comments