WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU AMETOA ONYO KWA WATUMISHI WA AFYA WANAOTOZA GHARAMA ZA MATIBABU WANANCHI WENYE KADI ZA BIMA YA CHF.

TAREHE 07-12-2017



Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa watumishi wa afya hapa nchini wanaotoza gharama za matibabu wananchi ambao wana kadi za bima ya afya ya jamii CHF.

Mh Ummy ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Humekwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati wa kampeni ya usafi wa mzingira na afya,ambapo amesema kuwa mwananchi mwenye kadi ya CHF anatakiwa kupata matibabu bure bila usumbufu.

Amesema kuwa kuanzia sasa mtumishi yeyote wa afya atakaye mtoza mwananchi mwenye kadi ya CHF fedha atachukuliwa hatua kali za kisheria na amewataka wananchi wote wenye kadi ya bima ya afya kutoa taarifa pale watakapodaiwa fedha kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ili wahusika waweze kushughulikiwa.

Ameongeza kuwa mikakati ya serikali ni kuhakikisha wananchi wote wa Tanzania wanapata huduma bora za matibabu na ndio maana bajeti ya wizara imeongezeka hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni mia mbili,hivyo ni vyema watumishi wote wa afya wakafuata sheria katika kazi zao za kuwahudumia wananchi.

Hata hivyo kampeni ya kitaifa ya afya na  usafi wa mazingira ya nipo tayari awamu ya pili inazinduliwa leo  na makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan.
WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU AMETOA ONYO KWA WATUMISHI WA AFYA WANAOTOZA GHARAMA ZA MATIBABU WANANCHI WENYE KADI ZA BIMA YA CHF. WAZIRI  WA AFYA MH. UMMY MWALIMU  AMETOA ONYO KWA WATUMISHI  WA AFYA WANAOTOZA GHARAMA ZA MATIBABU  WANANCHI WENYE KADI ZA BIMA YA CHF. Reviewed by safina radio on December 07, 2017 Rating: 5

No comments