MAANDANO YAZIDI HUKO MASHARIKI YA KATI.
TAREHE 12-12-2017
Eneo la mashariki ya
kati limeshuhudia siku ya tano ya maandamano leo kuhusiana na tangazo la rais
Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, wakati shutuma
nyingine zaidi zimetolewa kufuatia hatua hiyo yenye utata.
Wakati mamia kwa
maelfu ya waandamanaji wakijikusanya nchini Lebanon , waziri mkuu wa Israel
Benjamin Netanyahu amekutana na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya
mjini Brussels, akisema kwamba hatua hiyo inaleta uwezekano wa kupata amani.
Pia amesema anatarajia
wote ama mataifa mengi ya Umoja wa Ulaya yatafuata mfano wa Marekani , lakini
mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja huo Federica Mogherini amempinga kwa kusema
matarajio yake anaelekeza kwingine.
Mjini Cairo, rais
Vladimir Putin wa Urusi ameshutumu
uamuzi wa Trump na kusema unavuruga na kutoa wito wa kuanza tena kwa mazungumzo
yaliyokwama kwa muda mrefu.
MAANDANO YAZIDI HUKO MASHARIKI YA KATI.
Reviewed by safina radio
on
December 12, 2017
Rating:

No comments