RAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON AMEMTAKA WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU ATOE ISHARA YA KUTATUA MGOGORO NA WAPALESTINA .

TAREE 11-12-2017


Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amemtaka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu awe na ujasiri na atoe ishara kwa Wapalestina kwa lengo la kutatua mgogoro wa pande hizo mbili.

Katika mkutano wa viongozi hao na waandishi wa habari, Macron aliukosoa uamuzi wa rais wa Marekani ,Donald Trump wa kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel na kutoa mwito wa kuwepo kwa utulivu.

Macron amesema Ufaransa inataka suluhisho la nchi mbili zitakazoishi kwa amani ndani ya mipaka itakayotambuliwa kimataifa.

Kwa upande wake Netanyahu amesema Jerusalem haijawahi kuwa mji mkuu wa watu wengine wowote na kwamba Wapalestina watakapoutambua haraka ukweli huu ndipo pande hizo mbili zitakaposonga mbele katika kuleta amani.

 Netanyahu ameyasema hayo mjini Paris ambapo leo anatarajiwa kukutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, nchini Ubelgiji
RAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON AMEMTAKA WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU ATOE ISHARA YA KUTATUA MGOGORO NA WAPALESTINA . RAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON AMEMTAKA WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU  ATOE ISHARA YA KUTATUA MGOGORO NA WAPALESTINA . Reviewed by safina radio on December 11, 2017 Rating: 5

No comments