MAREKANI KUUTAMBUA JERUSALEM KAMA MJI MKUU WA ISRAEL
TAREHE 06-12-2017
Maafisa wa serikali ya Marekani
wamesema kuwa rais Donald Trump, leo atautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu
wa Israel.
Ikulu ya White House imethibitisha
kuwa rais Donald Trump pia atazungumza kuhusu juu ya kutangaza rasmi kuhamishia
kwa ubalozi wa Marekani Jerusalem.
Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya
white house sarah sanders amesema kuwa Trump alizungumza na baadhi ya viongozi
siku ya jumanne kuhusu mipango yake ya kuhamishia ubalozi huo kutoka Tel Aviv
kuupeleka Jerusalem.
Wakati huo huo viongozi wa
Palestina, Misri, Jordan na Saudi Arabia, wametoa onyo kwa rais Trump kuwa
kuhamishia ubalozi huo Jerusalem kutadhoofisha kabisa juhudi za kuleta amani
mashariki ya kati.
MAREKANI KUUTAMBUA JERUSALEM KAMA MJI MKUU WA ISRAEL
Reviewed by safina radio
on
December 06, 2017
Rating:

No comments