MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AMETAKA JITIADA MBALIMBALI ZIFANYIKE KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

TAREHE 01-12-2017


Makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan ametaka jitihada mbalimbali kufanyika ili kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana hapa nchini.

Mh Suluhu ameyasema hayo leo wakati akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika kitaifa jijini Dar-es-salaam,ambapo amesema kuwa endapo juhudi za ziada zitafanywa kati ya serikali,taasisi binafsi pamoja na wananchi kupambana na ugonjwa huo idadi ya vijana wanaoathirika na ukimwi itapungua kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuwa,inasikitisha kuona idadi ya waathirika wengi wa maambukizi ya virusi vya ukimwi ni wasichana wadogo,ambapo pia ametumia maadhimisho hayo kuwaonya wababa na wazee wanaowarubuni wasichana hao ili washiriki nao vitendo vya ngono kuacha tabia hiyo mara moja kwani watakapobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi hapa nchini TACAIDS Dr Leonad Maboko amesema kuwa licha ya maambukizi hayo kupungua hapa nchini bado kuna changamoto kwa vijana katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika maadhimisho hayo pia makamu wa rais alizindua taarifa ya maambukizi wa virusi vya ukimwi,ambapo mikoa ya Njombe na Iringa ndio inayoongoza kwa asilimia kubwa ya watu waloathirika na ugonjwa huo.


Hata hivyo maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani huadhimishwa kila ifikapo Desemba Mosi ya kila mwaka,ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Changia Mfuko wa Udhamini wa Ukimwi Okoa Maisha.
MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AMETAKA JITIADA MBALIMBALI ZIFANYIKE KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI MAKAMU  WA  RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AMETAKA JITIADA  MBALIMBALI ZIFANYIKE  KUPUNGUZA  MAAMBUKIZI  YA UKIMWI Reviewed by safina radio on December 01, 2017 Rating: 5

No comments