RAIS WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KAMPUNI YA TOTAL MUMAN NGUWERE
TAREHE 05-12-2017
Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamezungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Pombe
Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa kampuni ya TOTAL Muman
Nguwere ikulu jijini Dar-es-salaam.
Katika mazungumzo hayo rais Magufuli na mgeni wake
wamejadili masuala mbalimbali kuhusu kazi za kampuni ya Total na utafiti wa
mafuta unaofanywa na kampuni hiyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Wakizungumza mara baada ya mazungumzo hayo waziri wa viwanda
na biashara Mh Charles Mwijage na waziri wa nishati Mh Mernad Kaleman wamesema
kuwa mikakati ya uwekezaji unaofanywa na kampuni ya Total hapa nchini utasaidia
kukuza sekta ya viwanda hapa nchini pamoja na sekta ya nishati.
Katika hatua nyingine rais John Magufuli amekutana na
kufanya mazungumzo na balozi wa umoja wa Falme za Kiarabu Abdulah Ibrahim Al
Swaid na ujumbe wake.
Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamezungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano
RAIS WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KAMPUNI YA TOTAL MUMAN NGUWERE
Reviewed by safina radio
on
December 05, 2017
Rating:

No comments