SERIKALI IMEWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA.
Serikali imewataka watumishi wote wa uma hapa nchini
kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa ufanisi ili waweze kufikia hazima ya serikali ya awamu
ya tano ya kukuza uchumi wake kwa njia
ya viwanda.
Hayo yamesemwa leo na naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii
jinsia wazee na watoto Dr.Faustine Ndugulile,wakati akizungumza na wafanyakazi
wa taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru mkoani
Arusha,ambapo amesema kuwa ili hazma
ya kukuza uchumi wa nchi kwa njia ya viwanda ifanikiwe ni lazima kila
mfanyakazi afanye kazi kwa bidii.
Aidha Dr Ndugulile amesema kuwa taasisi ya maendeleo
ya jamii Tengeru ndio chachu ya wataalamu ambao majukumu yao ni kuhakikisha kwamba wanaisaidia serikali kuamsha hari ya wananchi
kwa kushiriki kwao katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya maendeleo
ya jamii Tengeru Dr,Patrick Golwite ameahidi kufanyia kazi maelekezo yote
yaliyotolewa na naibu waziri ikiwa ni
pamoja na kulipatia ufumbuzi tatizo la mpaka kati ya chuo cha mifugo na taasisi
ya maendeleo ya jamii Tengeru.
SERIKALI IMEWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA.
Reviewed by safina radio
on
December 15, 2017
Rating:
No comments