UJERUMANI YALAANI KITENDO CHA KUCHOMWA MOTO BENDERA YA ISRAEL
TAREHE 12-12-2017
Serikali ya Ujerumani
imelaani kitendo cha kuichoma moto bendera ya Israel kilichofanywa na watu
walioshiriki katika maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina mjini Berlin na
kupinga uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuutambua Jerusalem kuwa ni
mji mkuu wa Israel.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema
serikali yake inapinga aina zote za chuki dhidi ya Wayahudi na wageni.
Kansela Merkel
ameeleza kwamba hakuna tofauti zozote za mitazamo zinazoweza kuhalalisha
vitendo kama hivyo hata ikiwa ni kuhusu suala la mji wa Jerusalem.
Waziri wa Mambo ya
Ndani Thomas de Maizière na wa Mambo ya Nje, Sigmar Gabriel wametamka kuwa
vitendo kama hivyo haviwezi kuvumiliwa.
Hata ivyo Baraza kuu
la Wayahudi nchini Ujerumani limeelezea wasiwasi wake juu ya matukio ya
kuchomwa moto bendera ya Israel.
UJERUMANI YALAANI KITENDO CHA KUCHOMWA MOTO BENDERA YA ISRAEL
Reviewed by safina radio
on
December 12, 2017
Rating:

No comments