MKUU WA MKOA WA TABORA AGREY MWANRY AKABIDHI MAONI KWA MKUU WA POLISI IGUNGA.

TAREHE 20-12-2017




Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw Agrey Mwandry amemkabidhi mkuu wa polisi wa wilaya ya Igunga kura za maoni zenye majina ya watu wanaojihusisha na vitendo vya uhujumu wa miondombinu ya umeme wilayani humo.

Bw Mwandry amekabidhi majina hayo baada ya kuendesha kura ya maoni katika vitongoji vya Mkongoro na Makomelo katika mji mdogo wa Igunga kutokana na kuibuka kwa vitendo vya kuhujumu njia kuu za usambazaji umeme ujulikanao kama Back Bone inayopita katika vitongoji hivyo.

Pia Bw Mwandry amemwagiza mkuu huyo wa polisi wa wilaya ya Igunga kwenda kutumia majina hayo kama chanzo cha upelelezi ili kujua ni nani anayehusika na vitendo hivyo vya uharibifu wa miundombinu ya umeme ambayo serikali inatumia gharama kubwa kuitekeleza.


Nao wataalamu wa umeme kutoka shirika la umeme hapa nchini mkoani Tabora na makao makuu wamewaonya wanachi kuacha kuhujumu miundombinu hiyo kwani kwa kufanya hivyo wataathiri maisha yao na maendeleo ya nchi kiujumla.
MKUU WA MKOA WA TABORA AGREY MWANRY AKABIDHI MAONI KWA MKUU WA POLISI IGUNGA. MKUU WA MKOA WA TABORA AGREY MWANRY AKABIDHI MAONI KWA MKUU WA POLISI IGUNGA. Reviewed by safina radio on December 20, 2017 Rating: 5

No comments