TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA

TAREHE 13-12-2017


Thomas LemarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionThomas Lemar

Chelsea wanajiandaa na ofa ya pauni milioni 80 kumsaini mchezaji wa Monaco raia wa Ufaransa Thomas Lemar, 22, ambye alikuwa pia anamezewa mate na Liverpool na Arsenal mwezi Agosti. (L'Equipe, kupitia Daily Mail)
Meneja wa West Ham David Moyes anatathmini kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Arsenal, Jack Wilshere, 25. (Guardian)
Mlinzi wa Juventus Alex Sandro, 26, ambaye anamezewa mate na Manchester United, amekiambia klabua hiyo ya Italia kuwa angependa kuondoka lakini angependa alekee Chelsea mwezi Januari. (Sun)

Antoine GriezmannHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAntoine Griezmann

Mchezaji ambaye amekuwa akitafutwa kwa siku nyingi na Manchester Unites Antoine Griezmann, 26, anatarajiwa kuihama Atletico Madrid kwenda Barcelona msimu ujao. (Independent)
Arsenal tayari wamefikia makubaliano ya pauni milioni 35.3 kumsaini mchezaji wa Sevilla Steven Nzonzi mwezi Januari. (Gol kupitia Daily Mirror)
Pep Guardiola anaamini kuwa atahitaji kumsaini mlinzi mwezi Januari la sivyo Manchester City watakuwa matatani. (Guardian)

Thomas MeunierHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionThomas Meunier

Mchezaji wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 26, amehusishwa na kutaka kwenda Manchester United miezi ya hivi karibuni ameandika kwenye twitter kuwa angependa kuhamia Old Trafford. (Daily Express)
Winga wa zamani wa Everton Gerard Deulofeu, 23, ataondoka Barcelona kwenda Napoli kwa mkopo baada ya kushindwa kuwa katika kikosi cha kwanza huko Nou Camp. (Rai Sport kupitia Talksport)
Barcelona wanakaribia kukamilisha mpango wa kumsaini mlinzi wa Palmeiras raia wa Colombia Yerry Mina, 23, ambaye anaonekana kuwa atachukua mahala pake Javier Mascherano, 33. (AS)
TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA Reviewed by safina radio on December 13, 2017 Rating: 5

No comments