WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI NA UTAWALA BORA MH. GEORGE MKUCHIKA ATOA MAAGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZOTE HAPA NCHINI.
TAREHE 12-12-2017
Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi na utawala
bora Mh George Mkuchika amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote hapa nchini
kuwafukuza kazi wafanyakazi wote wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini TASAF
walioshiriki kuingiza majina ya watu ambao hawastahili kusaidiwa na mfuko huo.
Mh Mkuchika ameyasema hayo mkoani Tanga wakati akizungumza
na viongozi wa mkoa huo wakiwemo watendaji wa TASAF,ambapo amesema kuwa lengo
na mpango wa mfuko huo ni kunufaisha kaya maskini hivyo serikali haitawavumilia
wale wote wanaoenda kinyume na malengo hayo.
Amesema kuwa pamoja na nia njema ya kuanzishwa kwa
mfuko wa TASAF hapa nchini kuna baadhi ya watu wanaoharibu sifa za mfuko huo
kwa kusajili watu ambao hawakustahili kusahiliwa kutokana na sheria kukiukwa na
rushwa kutamalaki jambo linalosababisha watu wanyonge kukosa haki zao za
msingi.
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Tanga
Mhandisi Zela Said amesema kuwa hadi sasa kaya elfu hamsini na tano mia saba na
arobaini na tatu zimenufaika na mpango huo wa kunusuru kaya maskini mkoani
humo.
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI NA UTAWALA BORA MH. GEORGE MKUCHIKA ATOA MAAGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZOTE HAPA NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
December 12, 2017
Rating:

No comments