WAZIRI MKUU WA TANZANIA MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AMESEMA SERIKALI IMEWEKA MAZINGIRA MAZURI YA UPATIKANAJI WA VIWANJA KWA AJILI YA UJENZI.
TAREHE 07-12-2017
Waziri mkuu wa
jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema kuwa
serikali imeweka mazingira mazuri ya kuwezesha upatikanaji wa viwanja kwa ajili
ya ujenzi wa ofisi za mashirika mbalimbali ya Kimatifa mkoani Dodoma.
Mh majaliwa
ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa ofisi za umoja wa
mataifa,ambapo amesema kuwa uzinduzi wa ofisi hizo ni ishara za kuunga mkono
jitihada za serikali za kuhamia Dodoma.
Amesema kuwa mbali
na serikali kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa ofisi za
mashirika hayo pia itatoa msaada wa huduma za namna ya kuanzisha ujenzi wake
hivyo kwa mashirika ambayo yako tayari wawasiliane na meya wa manispaa ya
Dodoma ili wapate viwanja hivyo.
Ameongeza kuwa kwa
kutambua kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi sherehe zote za kitaifa ikiwemo za
uhuru kuanzia sasa zitaanza kufanyika mkoani Dodoma.
Kw upande wake
waziri wa mambo ya nje ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na mataifa
Balozi Agustine Mahiga amesema kuwa,wizara yake itasaidia kuwezesha juhudi za
serikali kuhamia Dodoma pamoja na kusimamia amani ili kuleta maendeleo kwa watu
wake.
WAZIRI MKUU WA TANZANIA MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AMESEMA SERIKALI IMEWEKA MAZINGIRA MAZURI YA UPATIKANAJI WA VIWANJA KWA AJILI YA UJENZI.
Reviewed by safina radio
on
December 07, 2017
Rating:

No comments