MKUU WA MKOA WA MOROGORO ATOA ONYO KWA WAZAZI WANAOWAACHISHA WATOTO WA KIKE SHULE MKOANI HUMO.
TAREHE 15-12-2017
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Steven Kebwe amewakemea
vikali hususani wazazi wa jamii ya kimaasai kwa kitendo cha kuwakatisha masomo
watoto wa kike na kuwaozesha ambapo amesema hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi ya watakaokamatwa wakijihusisha na vitendo hivyo.
Dk. Kebwe ametoa agizo hilo akiwa katika viwanja vya
shule ya sekondari Parakuyo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, wakati akiongoza
zoezi la kuchangisha fedha za ujenzi wa
bweni la wasichana wa shule hiyo ambapo asilimia kubwa ya wanafunzi katika shule
hiyo wanatoka katika jamii ya wafugaji ya kimasai.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kumekuwa na mchezo
mchafu kwa jamii za wafugaji kuwaachisha shule watoto wa kike na kuwaozesha jambo ambalo halikubaliki katika
uongozi wake na kumwagiza mkuu wa Wilaya ya Kilosa kusimamia kwa karibu maagizo
hayo.
Aidha amewataka wazee kuacha mara moja tabia ya kuoa
watoto wadogo na badala yake kuwaacha waende shule na kuongeza kuwa
atakayekiuka maagizo hayo sheria itachukua mkondo wake bila kujali umri wa
mhusika.
MKUU WA MKOA WA MOROGORO ATOA ONYO KWA WAZAZI WANAOWAACHISHA WATOTO WA KIKE SHULE MKOANI HUMO.
Reviewed by safina radio
on
December 15, 2017
Rating:

No comments