MOURINHO ATAKIWA KUTOA UFAFANUZI WA MATAMSHI YAKE.

TAREHE 15-12-2017

Manchester United manager Jose MourinhoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametakiwa kufafanua aliyoyasema kabla ya mechi ya Jumapili ambapo walilazwa na Manchester City 2-1 uwanjani Old Trafford.
Chama cha Soka England (FA) kimemtaka Mreno huyo kufafanua zaidi kuhusu aliyoyasema katika kikao cha kabla ya mechi Ijumaa akizungumza na wanahabari.
Mourinho alidai wachezaji wa City huanguka kwa urahisi sana.
Mourinho amepewa hadi saa 18:00 GMT siku ya Jumatatu kutoa ufafanuzi huo na FA.
Mourinho, 54, alisema pia kwamba hafikiri kama  angeruhusiwa kutoa ujumbe wa kisiasa akiwa pembeni mwa uwanja kama alivyofanya Guardiola.
Pep Guardiola majuzi alivalia utepe wa manjano - ishara ya kulalamika dhidi ya kufungwa kwa wanasiasa waliokuwa wanatetea uhuru wa jimbo la Catalonia, Uhispania.
Pep anatokea eneo hilo la Catalonia.
United walishindwa kwenye dabi hiyo na City wakaweka mwanya wa alama 11 kati yao na United kileleni Liig ya Premia.
Mourinho aidha alimwagiwa maziwa nje ya vyumba vya kubadilishia mavazi vya wachezaji Old Trafford baada yake kulalamika kwamba wachezaji wa City walikuwa wanasherehekea ushindi huo kupita kiasi.
MOURINHO ATAKIWA KUTOA UFAFANUZI WA MATAMSHI YAKE. MOURINHO ATAKIWA KUTOA UFAFANUZI WA MATAMSHI YAKE. Reviewed by safina radio on December 15, 2017 Rating: 5

No comments