WATU WENYE ULEMAVU WAMETAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA SHUGHULI ZAO NA ZA UJENZI WA TAIFA.

TAREHE 05-12-2017                                                      

Shirikisho la watu wenye ulemavu SHIVIWATA hapa nchini mkoani Rukwa limewataka watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika shughuli zao pamoja na za ujenzi wa taifa.

Wito huo umetolewa na katibu mkuu wa shirikisho hilo Bi Elina John wakati akizungumza katika maadhimisho ya watu wenye ulemavu mkoani humo,ambapo amewataka walemavu hao kuacha kujitenga kushiriki katika shughuli za kijamii kwa madai ya kuwa walemavu.

Bi Elina amesema kuwa,endapo walemavu watashiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo wataweza kujipatia kipato na kujikwamua katika hali ya umaskini ikiwa ni pamoja na kuondoa dhana ya kwamba mlemavu hawezi kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa.


Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Rukwa Bw Godfrey Mapunda amesema kuwa kuna haja ya kufahamu takwimu sahihi za watu wenye ulemavu hapa nchini ili kuwezesha serikali kupanga bajeti yao.
WATU WENYE ULEMAVU WAMETAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA SHUGHULI ZAO NA ZA UJENZI WA TAIFA. WATU WENYE ULEMAVU  WAMETAKIWA  KUSHIRIKI KIKAMILIFU  KATIKA SHUGHULI ZAO NA ZA UJENZI WA TAIFA. Reviewed by safina radio on December 05, 2017 Rating: 5

No comments