WATU 15 WANYONGWA NCHINI MISRI.

Serikali ya Misri imewanyonga watu 15 waliotiwa hatiani kwa mauaji ya wanajeshi tisa mwaka 2013 katika jimbo la Sinai kaskazini mwa nchi hiyo.

Mahakama ya kijeshi iliyokuwa ikisikiliza mashitaka dhidi ya walalamikaji ilitupilia mbali rufaa yao na kuunga mkono hukumu ya awali.

Watu hao walitiwa hatiani kwa kuhusika na mauaji ya Sajenti mmoja wa jeshi na wanajeshi wengine saba katika rasi ya Sinai miaka minne iliyopita. 

Misri imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi yanayofanywa na makundi ya itikadi kali mengi yakivilenga vikosi vya usalama na jamii ya wakristo wachache tangu mapinduzi yaliyofanywa na jeshi kumuondoa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi mwaka 2013.


Novemba mwaka huu zaidi ya waumini 300 waliuawa katika msikiti mmoja kaskazini mwa Sinai likiwa ni shambulizi baya zaidi la hivi karibuni katika historia ya nchi hiyo.
WATU 15 WANYONGWA NCHINI MISRI. WATU 15 WANYONGWA NCHINI MISRI. Reviewed by safina radio on December 27, 2017 Rating: 5

No comments