WATANZANIA WASHAURIWA KUJENGA MADHABAHU YA MUNGU ILI KUTEKA MALANGO YA MAFANIKIO.
Zikiwa
zimebaki siku chache kumaliza mwaka 2017 Watanzania wameshauriwa kujenga
madahabahu ya Mungu katika mwaka mpya 2018 ili kuteka malango ya mafanikio yao
na kuishi bila kusumbuliwa na magonjwa,umaskini pamoja na nguvu za giza.
Redio safina
kesho katika ukumbi wa maombi ulioko mbauda jijini Arusha kuanzia saa mbili
asubuhi hadi saa sita na nusu mchana itawafundisha watu umuhimu wa kuteka mwaka
na kufikia malengo kwa kuujengea madhabahu ya Mungu.
Aidha kulingana na somo hilo imebainika kuwa mafanikio
ya mtu kimaisha hutegemea nguvu ya madhabahu iliyomshikilia nafsi yake ambapo
mengine humfunga mtu asiweze kufanikiwa kiuchumi na kiroho.
Pia mafundisho
hayo yatakwenda sambamba na watu kufundishwa namna ya kujenga madhabahu ya Mungu
kwenye shughuli zao za kila siku kama vile kilimo na ufugaji,elimu na
biashara,vipawa na karama pamoja na huduma kwa ujumla.
Hata hivyo
watu watapaswa kuja na kalenda mpya ya mwaka wa 2018 ambapo maombi rasmi yatafanyika
ili watu waweze kuishi kwa amani bila kukumbwa na majanga yoyote baada ya kubomoa
madhabahu ya miungu iliyojengwa na shetani ndani ya watu na kazi zao.
WATANZANIA WASHAURIWA KUJENGA MADHABAHU YA MUNGU ILI KUTEKA MALANGO YA MAFANIKIO.
Reviewed by safina radio
on
December 13, 2017
Rating:
No comments