WAZIRI JAFFO AMEMPA SIKU 20 MKANDARASI ANAYEJENGA WODI YA KINA MAMA KATIKA ZAHANATI YA MKUNZI.
TAREHE 12-12-2017
Waziri wa nchi
ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh Suleman Jaffo amempa siku
20 mkandarasi anayejenga wodi ya akina mama na watoto katika zahanati ya Mkunzi
iliyopo wilayani Muheza mkoani Tanga kukamilisha ujenzi huo.
Mh Jaffo ametoa
kauli hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo wilayani Muheza,ambapo amesema kuwa serikali inafanya kila
liwezekanalo kuboresha huduma za afya,hivyo mkandarasi huyo anatakiwa
kukamilisha wodi hiyo ili wananchi wapate huduma bora za matibabu.
Aidha amewataka
watendaji wa serikali kutumia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa
na serikali kwa matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Hata hivyo waziri
huyo amempongeza mkuu wa wilaya ya Muheza pamoja na viongozi wengine kwa kazi
kubwa wanayoifanya ya kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ya
kuhakikisha huduma za afya zinaendelea kuwa bora hapa nchini.
WAZIRI JAFFO AMEMPA SIKU 20 MKANDARASI ANAYEJENGA WODI YA KINA MAMA KATIKA ZAHANATI YA MKUNZI.
Reviewed by safina radio
on
December 12, 2017
Rating:

No comments