GORDON REID AFUZU NUSU FAINALI YA MASHINDANO YA WALEMAVU YA TENNIS MASTERS

TAREHE 01-12-2017

Gordon Reid anatarajiwa kupanda kwenye viwango vya kimataifa hivi karibuni
Image caption
Muingereza Gordon Reid ameshinda mchezo wake wa pili katika mashindano ya walemavu ya Tennis Masters na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye hatua ya nusu fainali itakayopigwa mjini Loughborough.
Baada ya kupoteza mbele ya bingwa Joachim Gerard siku ya Jumatano, Reid amemshinda Nicolas Peifer wa Ufaranda kwa seti 3-6 6-4 6-3.
Muingereza mwenzake Andy Lapthorne nae pia amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumchapa Heath Davidson wa Australia kwa seti 6-2 7-5.
Alfie Hewett naLucy Shuker walipoteza michezo yao.
Hewett, namba mbili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, alipangwa kucheza na Shingo Kunieda wa Japan lakini alipoteza kwa seti 2-6 6-4 6-2 baada ya kuumia bega.
GORDON REID AFUZU NUSU FAINALI YA MASHINDANO YA WALEMAVU YA TENNIS MASTERS GORDON REID AFUZU NUSU FAINALI YA MASHINDANO YA WALEMAVU YA TENNIS  MASTERS Reviewed by safina radio on December 01, 2017 Rating: 5

No comments

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.