SERIKALI KUENDELEA KUSAIDIA KAYA MASIKINI NCHINI.
TAREHE 05-12-2017

Serikali imesema
kuwa itaendelea kuzisaidia kaya mbalimbali hapa nchini kuondokana na hali ya
umaskini kupitia mfuko wake wa kusaidia kaya maskini wa TASAF.
Hayo yameelezwa na
mtendaji mkuu wa mfuko wa kusaidia kaya maskini hapa nchini wa TASAF Bw
Ladslaous Mwamanga wakati akielezea mafanikio ya mfuko huo mbele ya waandishi
wa habari jijini Dar-es-salaam,ambapo amesema kuwa juhudi kubwa za serikali ni
kuendelea kuwezesha kaya zote ambazo ziko kwenye hali ya umaskini uliokithiri
ili ziweze kujikimu na kupata mahitaji ya msingi.
Bw Mwamanga amesema
kuwa tangu mfuko wa TASAF uanze kazi zake ya kuwahudumia wananchi kaya nyingi
hapa nchini zimepiga hatua kutoka katika umaskini uliokithiri kuelekea kwenye
maendeleo na mafanikio makubwa.
Amesema mafanikio
ya TASAF ni mwendelezo wa kuwapa fursa walengwa wa mfuko huo kushiriki katika
sekta za maendeleo endelevu kwa manufaa yao binafsi na kwa taifa kwa ujumla.
SERIKALI KUENDELEA KUSAIDIA KAYA MASIKINI NCHINI.
Reviewed by safina radio
on
December 05, 2017
Rating:

No comments