WAZIRI TILLERSON ASEMA MAREKANI IKO TAYARI KWA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI.

TAREHE 13-12-2017
Rex Tillerson

Image caption


Image caption

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema Marekani iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote.
Taaarifa yake imeonekana kuwa tofauti na msimamo wa awali wa Marekani kuwa Korea Kaskazini ni lazima iharibu zana zake kabla ya mazungummzo yoyote kufanyika.
Lakini saa chache baadaye Ikulu wa White House ilisema msimamo wa  Trump kwa Korea Kaskazini haujabadilika, huku hatua ya Korea Kaskazini ya kuunda zana za nyuklia ikisababisha Marekani kuongeza vikwazo vikubwa dhidi ya nchi hiyo.

Kando na hilo mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibu alizuru Korea Kaskazini aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa Korean Kaskazini wanaamini kuwa ni muhimu kuzuia vita.
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini umeharibika kufuatia majaribio ya hivi karibuni ya mabomu ya nyuklia na makombora na kuwepo vita vya Maneno kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Hata hivyo akizungumza kwenye mkutano wa baraza la nchi za Atlantic siku ya Jumanne, Bw Tillerson alisema kuwa Marekani haiwezi kukubali Korea Kaskazini kujihami kwa silaha za nyuklia.


WAZIRI TILLERSON ASEMA MAREKANI IKO TAYARI KWA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI. WAZIRI TILLERSON ASEMA MAREKANI IKO TAYARI KWA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI. Reviewed by safina radio on December 13, 2017 Rating: 5

No comments