RAIS JACOB ZUMA AMEAMRIWA NA MAHAKAMA KUANZISHA UCHUNGUZI WA MADAI YA RUSHWA DHIDI YA SERIKALI.
TAREHE 14-12-2017
Mahakama kuu nchini
Afrika Kusini imemuamuru rais Jacob Zuma aanzishe uchunguzi katika kipindi cha
siku 30 juu ya madai ya rushwa dhidi ya serikali yake.
Mahakama hiyo imetoa
agizo hilo baada ya uchunguzi uliofanyika kufichua uhalifu wa kiwango cha juu
na ufisadi kutokana na uhusiano wa rais Zuma na familia ya Gupta wafanyabishara
matajiri wakubwa ambao wanatuhumiwa kupata kandarasi nono za serikali na kuwa
na ushawishi mkubwa katika maamuzi ya serikali.
Hata hivyo madai hayo yamekanushwa na rais
Zuma pamoja na familia ya Gupta.
Zuma amekuwa anashinikizwa ajiuzulu kutokana
na madai hayo.
RAIS JACOB ZUMA AMEAMRIWA NA MAHAKAMA KUANZISHA UCHUNGUZI WA MADAI YA RUSHWA DHIDI YA SERIKALI.
Reviewed by safina radio
on
December 14, 2017
Rating:

No comments